Mwa. 47:29-31 Swahili Union Version (SUV)

29. Siku za kufa kwake Israeli zikakaribia; akamwita mwanawe Yusufu, akamwambia, Kama nimeona kibali machoni pako, weka mkono wako chini ya paja langu, ukanifanyie rehema na kweli; nakusihi usinizike katika Misri.

30. Lakini nitakapolala pamoja na baba zangu, unichukue toka Misri, unizike katika kaburi lao. Akasema, Nitafanya kama ulivyosema.

31. Akanena, Niapie. Naye akamwapia. Israeli akajiinamisha kwenye mchago wa kitanda.

Mwa. 47