Mwa. 47:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo Yusufu akaja akamwarifu Farao, akasema, Baba yangu, na ndugu zangu, na kondoo zao, na ng’ombe zao, na yote waliyo nayo, wamekuja kutoka nchi ya Kanaani, nao wako katika nchi ya Gosheni.

2. Akatwaa watu watano miongoni mwa nduguze, akawasimamisha mbele ya Farao.

3. Farao akawauliza hao nduguze, Kazi yenu ni nini? Wakamwambia Farao, Watumwa wako tu wachunga wanyama, sisi, na baba zetu.

Mwa. 47