Mwa. 45:24-28 Swahili Union Version (SUV)

24. Akaagana na ndugu zake, wakaenda zao; naye akawaambia, Msigombane njiani.

25. Wakatoka Misri, wakafika nchi ya Kanaani kwa Yakobo, baba yao.

26. Wakampasha habari, wakisema, Yusufu angali hai; naye ndiye mtawala katika nchi yote ya Misri. Moyo wake ukazimia, kwa sababu hakuwasadiki.

27. Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyoyapeleka Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.

28. Israeli akasema, Yatosha! Yusufu mwanangu angali hai; nitakwenda, nionane naye kabla sijafa.

Mwa. 45