Mwa. 38:3-8 Swahili Union Version (SUV)

3. Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri.

4. Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani.

5. Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa.

6. Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari.

7. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; na BWANA akamwua.

8. Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao.

Mwa. 38