Mwa. 38:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira.

2. Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake.

3. Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri.

4. Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani.

5. Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa.

Mwa. 38