Mwa. 36:32-43 Swahili Union Version (SUV)

32. Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba.

33. Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake.

34. Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake.

35. Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi.

36. Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake.

37. Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake.

38. Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake.

39. Akafa Baal-hanani, mwana wa Akbori, akamiliki Hadadi badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.

40. Na hayo ndiyo majina ya majumbe waliotoka kwa Esau, kufuata jamaa zao, na mahali pao, kwa majina yao. Jumbe Timna, jumbe Alva, jumbe Yethethi,

41. jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni,

42. jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibsari,

43. jumbe Magdieli, jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu, kufuata makao yao, katika nchi ya mamlaka yao. Naye huyo ndiye Esau, baba ya Edomu.

Mwa. 36