25. Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana.
26. Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.
27. Na hawa ni wana wa Eseri, Bilhani, na Zaawani, na Akani.
28. Na hawa ni wana wa Dishani, Usi, na Arani.
29. Hawa ndio majumbe waliotoka katika Wahori; jumbe Lotani, jumbe Shobali, jumbe Sibeoni, jumbe Ana,
30. jumbe Dishoni, jumbe Eseri jumbe Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, kwa habari za majumbe yao, katika nchi ya Seiri.
31. Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli.
32. Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba.
33. Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake.