Mwa. 35:17-20 Swahili Union Version (SUV)

17. Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine.

18. Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.

19. Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu.

20. Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.

Mwa. 35