13. Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.
14. Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake.
15. Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.
16. Wakasafiri kutoka Betheli, hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito.