6. Wale wajumbe wakarudi kwa Yakobo wakisema, Tulifika kwa ndugu yako, Esau, naye anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye.
7. Ndipo Yakobo akaogopa sana, na kufadhaika sana, akawagawanya watu waliopo pamoja naye, na kondoo, na ng’ombe, na ngamia, wawe matuo mawili.
8. Akasema, Akija Esau kwa kundi la kwanza, akalipiga, kundi litakalosalia litaokoka.