Mwa. 30:7-9 Swahili Union Version (SUV)

7. Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili.

8. Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.

9. Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe.

Mwa. 30