21. Yakobo akamwambia Labani, Nipe mke wangu, maana siku zangu zimetimia; niingie kwake.
22. Labani akakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu.
23. Ikawa wakati wa jioni akamtwaa Lea, binti yake, akamletea Yakobo, naye akaingia kwake.
24. Labani akampa Lea mjakazi wake Zilpa, awe mjakazi wake.
25. Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda?
26. Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa;