Mwa. 27:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.

2. Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.

3. Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;

Mwa. 27