Mwa. 25:31-34 Swahili Union Version (SUV)

31. Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.

32. Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi?

33. Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

34. Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

Mwa. 25