1. Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura.
2. Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Sua.
3. Yokshani akamzaa Sheba, na Dedani; na wana wa Dedani walikuwa Waashuri na Waletushi, na Waleumi.
4. Na wana wa Midiani walikuwa, Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa.Hao wote walikuwa ni wana wa Ketura.
5. Ibrahimu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo.
6. Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu.
7. Hizi ndizo siku za miaka ya maisha ya Ibrahimu alizoishi, miaka mia, na sabini na mitano.
8. Ibrahimu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.
9. Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni bin Sohari Mhiti, lielekealo Mamre.