Mwa. 22:15-24 Swahili Union Version (SUV)

15. Malaika wa BWANA akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni

16. akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

17. katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

18. na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

19. Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.

20. Ikawa baada ya mambo hayo, Ibrahimu akaambiwa ya kwamba, Tazama, Milka naye amemzalia Nahori ndugu yako wana;

21. Usi, mzaliwa wa kwanza wake, na Buzi nduguye, na Kemueli, baba wa Aramu;

22. na Kesedi, na Hazo, na Pildashi, na Yidlafu, na Bethueli.

23. Bethueli akamzaa Rebeka; hao wanane Milka alimzalia Nahori ndugu wa Ibrahimu.

24. Na suria wake Reuma naye alizaa Teba na Gahamu na Tahashi na Maaka.

Mwa. 22