32. Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.
33. Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.
34. Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.