Mwa. 2:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.

2. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

3. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

4. Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa.Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na nchi

5. hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;

6. ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.

7. BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Mwa. 2