Mwa. 11:30-32 Swahili Union Version (SUV)

30. Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto.

31. Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.

32. Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.

Mwa. 11