Mwa. 11:19-31 Swahili Union Version (SUV)

19. Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia mbili na kenda, akazaa wana, waume na wake.

20. Reu akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi.

21. Reu akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, waume na wake.

22. Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa Nahori.

23. Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka mia mbili, akazaa wana, waume na wake.

24. Nahori akaishi miaka ishirini na kenda, akamzaa Tera.

25. Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia na kumi na kenda, akazaa wana, waume na wake.

26. Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani.

27. Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu.

28. Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo.

29. Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska.

30. Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto.

31. Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.

Mwa. 11