Mwa. 10:21-32 Swahili Union Version (SUV)

21. Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana.

22. Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu.

23. Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.

24. Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi.

25. Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani.

26. Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera,

27. na Hadoramu, na Uzali, na Dikla,

28. na Obali, na Abimaeli, na Seba,

29. na Ofiri, na Havila, na Yobabi. Hao wote ndio wana wa Yoktani.

30. Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki.

31. Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.

32. Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.

Mwa. 10