2. Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
3. Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
4. Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
5. Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
6. Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
7. Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
8. Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9. Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA.
10. Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
11. Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
12. na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.
13. Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
14. na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.
15. Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
16. na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi,
17. na Mhivi, na Mwarki, na Msini,
18. na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana.
19. Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.