2. Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
3. Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
4. Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
5. Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
6. Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
7. Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
8. Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9. Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA.
10. Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.