Mwa. 10:15-20 Swahili Union Version (SUV)

15. Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,

16. na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi,

17. na Mhivi, na Mwarki, na Msini,

18. na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana.

19. Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.

20. Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.

Mwa. 10