Mt. 9:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini kwao.

2. Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

3. Na tazama, baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru.

4. Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu?

5. Kwa maana rahisi ni lipi, ni kusema, Umesamehewa dhambi zako, au ni kusema, Ondoka, uende?

6. Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.

7. Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake.

Mt. 9