9. Basi ninyi salini hivi;Baba yetu uliye mbinguni,Jina lako litukuzwe,Ufalme wako uje,
10. Mapenzi yako yatimizwe,hapa duniani kama huko mbinguni.
11. Utupe leo riziki yetu.
12. Utusamehe deni zetu,kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13. Na usitutie majaribuni,lakini utuokoe na yule mwovu.[Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.Amina.]
14. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
15. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
16. Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
17. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
18. ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.