17. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
18. ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
19. Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
20. bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
21. kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.