Mt. 5:41-48 Swahili Union Version (SUV)

41. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.

42. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

43. Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44. lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

45. ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

46. Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

47. Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?

48. Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Mt. 5