Mt. 4:7-17 Swahili Union Version (SUV)

7. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

8. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,

9. akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.

10. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

11. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.

12. Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;

13. akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;

14. ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,

15. Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,Njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani,Galilaya ya mataifa,

16. Watu wale waliokaa katika gizaWameona mwanga mkuu,Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mautiMwanga umewazukia.

17. Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Mt. 4