6. akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa,Atakuagizia malaika zake;Na mikononi mwao watakuchukua;Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
8. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9. akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
10. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
11. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
12. Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;