4. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
5. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
6. akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa,Atakuagizia malaika zake;Na mikononi mwao watakuchukua;Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
8. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9. akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
10. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.