Mt. 4:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.

2. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.

3. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.

4. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

Mt. 4