Mt. 27:64-66 Swahili Union Version (SUV)

64. Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza.

65. Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo.

66. Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi.

Mt. 27