Mt. 27:15-18 Swahili Union Version (SUV)

15. Basi wakati wa siku kuu, liwali desturi yake huwafungulia mkutano mfungwa mmoja waliyemtaka.

16. Basi palikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, aitwaye Baraba.

17. Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo?

18. Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda.

Mt. 27