1. Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
2. wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa liwali.
3. Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.
4. Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.
5. Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.