Mt. 26:5-13 Swahili Union Version (SUV)

5. Lakini wakasema, Isiwe wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia katika watu.

6. Naye Yesu alipokuwapo Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,

7. mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani.

8. Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakasema, Ni wa nini upotevu huu?

9. Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini.

10. Yesu akatambua akawaambia, Mbona mnamtaabisha mwanamke? Maana ni kazi njema aliyonitendea mimi.

11. Kwa maana siku zote mnao maskini pamoja nanyi; lakini mimi hamnami siku zote.

12. Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hiyo, ametenda hivyo ili kuniweka tayari kwa maziko yangu.

13. Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake.

Mt. 26