3. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;
4. bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.
5. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.
6. Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.
7. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.
8. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.
9. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
10. Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
11. Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
12. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
13. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
14. Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.
15. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
16. Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.
17. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.
18. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake.
19. Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.