2. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.
3. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;
4. bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.
5. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.