46. Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.
47. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
48. Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;
49. akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi;
50. bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,
51. atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.