40. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
41. wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa.
42. Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.
43. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
44. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.
45. Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?