Mt. 24:4-10 Swahili Union Version (SUV)

4. Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.

5. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.

6. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.

7. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.

8. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.

9. Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.

10. Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.

Mt. 24