Mt. 23:3-7 Swahili Union Version (SUV)

3. basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.

4. Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.

5. Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;

6. hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,

7. na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.

Mt. 23