1. Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema,
2. Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa;
3. basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.
4. Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.