38. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
39. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
40. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
41. Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?
42. Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.
43. Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,
44. Bwana alimwambia Bwana wangu,Uketi mkono wangu wa kuume,Hata niwawekapo adui zakoKuwa chini ya miguu yako?
45. Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?
46. Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.