32. Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai.
33. Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake.
34. Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja.
35. Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
36. Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
37. Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
38. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
39. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
40. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
41. Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?
42. Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.
43. Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,