27. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.
28. Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
29. Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
30. Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.
31. Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema,
32. Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai.
33. Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake.
34. Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja.
35. Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu;
36. Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?