35. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe.
36. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza wakawatenda vile vile.
37. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu.
38. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.
39. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua.
40. Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu, atawatendaje wale wakulima?
41. Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.
42. Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko,Jiwe walilolikataa waashi,Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni;Neno hili limetoka kwa Bwana,Nalo ni ajabu machoni petu?