Mt. 21:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia,

2. Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye; wafungueni mniletee.

3. Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.

4. Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,

5. Mwambieni binti SayuniTazama, mfalme wako anakuja kwako,Mpole, naye amepanda punda,Na mwana-punda, mtoto wa punda.

Mt. 21