Mt. 20:27-34 Swahili Union Version (SUV)

27. na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;

28. kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.

29. Hata walipokuwa wakitoka Yeriko mkutano mkubwa wakamfuata.

30. Na tazama, vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, walipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi!

31. Mkutano wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi!

32. Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini?

33. Wakamwambia, Bwana, twataka macho yetu yafumbuliwe.

34. Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; mara wakapata kuona, wakamfuata.

Mt. 20