3. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
4. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
5. Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
6. Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda;Kwa kuwa kwako atatoka mtawalaAtakayewachunga watu wangu Israeli.